Book Detail

TOBA by Mai Godfrey

TOBA

by Mai Godfrey

Pages: 466

Dimensions: 5 x 8

Category
  • RELIGION - Prayer
  • RELIGION - Christian Life - Inspirational
  • RELIGION - Christian Life - General

Type : Paperback

ISBN : 9781662894558

Price : $24.49Toba. Inamaana gani kwako?
Inakuletea hali ya hofu? Au inakuletea hali ya furaha?
Umeshawahi kujikuta kwenye hali ya ukavu wa kiroho ukajisikia kuwa mtupu, haijalishi nini unafanya? Iwe ni kwenda kanisani kwa ujumla, au kusali kwa kujilazimisha, chochote unachokifanya juu ya mambo ya rohoni huvutiwi nayo, hata kuomba kwako ni pasipo kuwa na msukumo wa ndani na kuishia kujisikia vibaya? Kama ndivyo hiki ni kitabu kitakachokufaa.
Kitabu cha Toba cha mwandishi Mai Godfrey ni cha kipekee na chenye kukupa mwanga kwa habari ya Toba. Msomaji utakutana na kitabu chenye utaratibu muhimu wa kufanya toba, unaomsaidia mtu yeyote kuweza kuutafuta uso wa Mungu. Kitabu hiki kinaweza kuwasaidia wakristo na wasiowakristo kumjua Mungu wa kweli kwa namna tofauti baada ya kufanya toba. Ni muongozo unaoweza kutumika tena na tena, iwe ni kwa ajili ya toba tu au kwa ajili ya maombi mazuri ya kupambana na vita vya kiroho na kufunguliwa. Muongozo wake utakusaidia kuweza kuomba kwa nguvu na mamlaka na kuweza kuona matokeo unayotamani kuyapata unapoomba.
Ndani ya kurasa hizi, msomaji na muombaji, utakutana na shehena kubwa ya sala zenye maelezo ya kina juu ya huduma ya mwandishi, mpangilio wake, dira yake, pamoja na shuhuda zenye uzito wa majibu ya maombi. Unapokitumia kitabu hiki, unatengeneza mahusiano yako na Mungu, pamoja na watu wanaokuzunguka. Miujiza iliyokuwa inaonekana haiwezekani, mara itaonekana kuwezekana. Anza safari yako ya kuwa muombaji mzuri leo!

Search by Topic

Browse By New Releases